We’ve updated our Terms of Use to reflect our new entity name and address. You can review the changes here.
We’ve updated our Terms of Use. You can review the changes here.

Tunakushukuru Mama Maria

by La Mennais Choir Moshi (Tanzania)

/
  • Streaming + Download

    Includes unlimited streaming via the free Bandcamp app, plus high-quality download in MP3, FLAC and more.
    Purchasable with gift card

      €4 EUR  or more

     

1.
Chorus: Tunakushukuru mama Maria (Kwa neema) kwa neema unazotujalia (Asante) Asante Mama wa Yesu uliye na huruma (uzidi) kutuombea mpaka saa ya kufa. 1. Mama Maria Mama mfariji wetu, Asante sana kwa kutusimamia. Chorus (1x) 2. Maombezi yako yatutia nguvu, Asante Mama Maria mtakatifu. Lyrics: Chorus (1x) 3.Tuna furaha, tuna matumaini, Kwa kuwa tu nawe Mama wa huruma. Chorus (1x) 4.Mama wa Yesu, Ewe Mama Maria, Tusaidie, tushinde vishawishi. Chorus (1x) 5.Katika uwingu ndiwe mbarikiwa, Katika maisha ndiwe kinga yetu. Chorus (1x)
2.
Lyrics: Chorus: (2x) Bwana atatufunika kwa manyoya yake, Bwana atatufunika kwa manyoya yake, Chini chini (3x) Ya mbawa zake, tutapata kimbilio. 1. Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana. Chorus (2x) 2. Maana yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo. Chorus (2x) 3.Nita sema bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakae mtumaini. Chorus (2x)
3.
Nani Ni Nani 02:38
Lyrics: Chorus: (1x) Nani ni nani? Nani ni nani? Nani ni kama mungu, Mwenye uweza na mwenye ukuu, Nani ni nani? Nani kama mungu. Mwenye uweza na mwenye ukuu, Nani ni nani? Nani kama mungu. 1.Amelilinda mchana kutwa niseme nini? Ni nani kama mungu? Chorus (1x) 2.Ameniumba jinsi nilivyo, nipendezavyo. Ni nani kama mungu? Chorus (1x) 3.Niimbee nini? Nisifu nini? Niseme Nini? Ni nani kama mungu? Chorus (1x)
4.
Lyrics: 1. Nimeonja pendo lako, nimejua u mwema nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe. Nitawaongoza vyema waimbe kwa furaha, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe. Chorus: (1x) Ukarimu wako (Bwana), Na huruma wako (Wewe), Msamaha wako (Bwana), Na upole wako (Wewe), Umenitendea wema usiopimika, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe. 2.Kina mama simameni piga vigelegele, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe, Kina baba nyanyukeni mkapige makofi, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe. Chorus (1x) 3. Watu wote nesanesa chezeni kwa furaha, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe, Inua mikono juu shangilieni bwana, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe. Chorus (1x) 4. Watawa washangilieni na makasisi waimbe, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe, Walei warukeruke waseme aleluya, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe. Chorus (1x) 5.Vitambaa mikononi vipeperushwe juu, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe, Na vichwa viyumbe yumbe kwa mwendowa kuringa, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe. Chorus (1x) 6.Nitakushukuru mimi na nyumba yangu yote, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe, Nitayatangaza haya maisha yangu yote, nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe.
5.
Lyrics: Chorus: (2x) Ndimi mtumishi wako nitafurahi kwako bwana, Ndimi mtumishi wako nitafurahi kwako bwana. 1.Nitajongea altare ya bwana, mungu wa raha na roho yangu. Chorus (2x) 2.Machoni pangu meza imepambwa, bwana tazama adui zangu. Chorus (2x) 3. Malishoni mwa majani mabichi, ananitunza nikiwa naye. Chorus (2x) 4.Sifa ziende kwa baba na mwana, Na kwake milele yote. Chorus (2x)
6.
Lyrics: Chorus: (2x) Mwili wako Yesu ni chakula kweli (na damu), Damu yako Yesu ni kinywaji kweli. 1.Mkate mtakitifu ni chakula safi, Kwa roho zetu kwa roho zetu. Chorus (2x) 2. Damu takatifu ni kinywaji safi, Kwa roho zetu kwa roho zetu. Chorus (2x) 3.Tuwe na imani ndiye Yesu kweli, Ni mungu wetu ni mungu wetu. Chorus (2x) 4.Tumwabudu hapa kwa heshima kubwa, Ni mwokozi wetu ni mwokozi wetu. Chorus (2x)
7.
Lyrics: 1. Laminee ndio chuo chetu, Cha mafunzo ya kuelimisha, Seremala na ushonaji, Computer na biashara. (2x) Chorus: (1x) Wanachuo, huko ndiko kujitegemea, Wanachuo, tuinue taaluma yetu, Wanachuo, huku ndiko kujitegemea, Tuboreshe, maisha yetu. 2. Lamennais ndio chuo chetu, Cha mafunzo ya kuelimisha, Maisha na kingereza, Ujenzi na makenika. (2x) Chorus (1x)
8.
Lyrics: Chorus: (1x) Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote, Nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana, Nilalapo nakuota wewe, Niamkapo ni heri mama we! Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote. 1. Tanzania Tanzania ninapokwenda safarini kutazama maajabu, Biashara nayo makazi, Sitaweza kusahau mimi mambo mema, Ya kwetu kabisa, Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Chorus (1x) 2. Tanzania Tanzania watu wako ni wema sana, Nchi nyingi zakuota nuru yako hukana tena, Nawageni wakukimbilia ngome yako imara kwelii we, Taniania Tanzania heri yako kwa mataifa. Chorus (1x) 3. Nchi nzuri Tanzania karibu wasio kwao, Wenye shida na taabu hukimbizwa na walowezi, Tanzania yawakaribisha mpigane kiume chema we, Tanzania Tanzania mola awe nawe daima. Chorus (1x)

about

The La Mennais Choir Moshi is an integral part of the La Mennais Vocational Training Centre in Moshi/ Tanzania (lamennaisvtc.org)

It was in 2006, that the Brothers of Christian Instruction in collaboration with their German friends of HELFEN MACHT SCHULE e.V. built a school at the Brothers’ Centre in Moshi (Tanzania). The school provides skills to disadvantaged youth, especially primary school leavers who could not pursue secondary education and form four dropouts. It intends to equip these youth with the needed knowledge to start self-reliant careers in the field of their choice.

Additionally to their theoretical and practical timetable in the centre, the students are offered extra-curricular activities, e.g. choir, sports or agriculture, which encourage them to develop their individual talents. These choir sessions took place during the evening in one of their class rooms.

70% of the benefits of this LP sale will directly go to the La Mennais Vocational Training Centre and support the choir and futher students activities

credits

released July 27, 2013

Credits:

Choir Master: Emmanuel Moshi & Josephine Riwa
Drums: Robert Mosha
Kayamba: Melikisedek Kessy

Choir members: Gerald Malunda, Credo Nwakanzi, Priscuss Abou, Bahat Mallya, Valence Lyimo, Amadeus Massawi, Emanueli R. Moshi, Artas Makoi, Evance Marenge, Dionisian Mallya, Alfonce Mtui, Bonifasi Shayo, Rogasian Ulassa, Colman Mushi, Amini Wirambowa, Nikasi Ngowi, Josephina Ntsuya, Krenki Kiria, Felix Kiria, Gabriel Mushi, Devota, Tesh, Jaclean Kessy, Jacklean Muya, Sapienisa Nyake, Julitha Tarimogea, Jackline Urio, Baltazar Renatus, Audifas Severini, Agripinus Kika, Amani Mwumbo, John Mkakanze, Melodi Shoo, Prisca Munish, Veronica Shayo

Recorded at La Mennais Vocational Training Centre in Moshi/ Tanzania
Songs produced by Thomas Mecha for SAUTI YA FURAHA
All songs mastered by Janis Kersting

Cover art by Thomas Mecha

license

all rights reserved

tags

about

Sauti Ya Furaha Nairobi, Kenya

Sauti ya Furaha was established in 2013 with the aim to spread beautiful, energetic and authentic African youth choral music. The name Sauti ya Furaha derives from Swahili language and means “Voice of Joy”.

We want to give African gospel music more visibility so that this music can reach as many people in the world as possible!

70% of the profit go directly to the young artists.
... more

contact / help

Contact Sauti Ya Furaha

Streaming and
Download help

Report this album or account

If you like Tunakushukuru Mama Maria, you may also like: